SEKTA YA FEDHA

UTANGULIZI

Sekta hii ilianzishwa mwaka 1996 ili kutoa huduma kwa wafanyakazi na wanachama waliopo katika Taasisi za Fedha kama benki, maduka ya kubadilisha fedha za kigeni, mifuko ya hifadhi ya jamii, mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), kampuni za bima na taasisi ndogo ndogo za fedha. Huduma hizo ni pamoja na; kujadili na kufunga Mikataba ya Hali Bora, kuhimiza uboreshaji wa mazingira mazuri ya kufanyia kazi, Kuhakikisha saa za kazi na mikataba bora ya ajira inatekelezwa

Kazi za Sekta

1. Kushiriki kikamilifu katika Mabaraza ya Wafanyakazi

2. Kuhamasisha na kuingiza wanachama wapya

3. Kushiriki katika mikutano mbalimbali ya wadau

4. Kuwakilisha wanachama katika utatuzi wa migogoro ya kikazi katika ngazi zote

5. Kutoa Elimu kwa Wanachama, Viongozi na Wafanyakazi juu ya Sheria za kazi na mbinu za majadiliano

6. Kujadili na kufunga mikataba ya hali bora (CBA) baina ya Chama na Waajiri

7. Kusimamia utekelezaji wa Mikataba, Maazimio na Matamko ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) yaliyoridhiwa na Nchi yetu

Mkuu wa Sekta ya Taasisi za Fedha, Adv. Peles Jonathan-Hageze (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB PLC Ndg. Abdul Majid Nsekela (kushoto) wakibadilishana Mkataba baada ya kutia sahihi Mkataba wa Hali Bora kati ya TUICO na CRDB Bank PLC