KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI

    Utangulizi

    Ukaguzi wa ndani ni kitengo kinachoshughulika na kutathimini,kupitia na kutoa maoni juu ya mambo ya uhasibu, fedha na uendeshaji wa Chama kwa ujumla

    Kazi za Kitengo

    1. Kupitia na kushauri Chama juu ya uimara wa mfumo wa uthibiti wa ndani hasa juu ya mapato na matumizi.

    2. Kufuatilia kama Chama kinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa,

    3. Kutambua na kutathmini athari mbalimbali ambazo zinaweza kuathiri na kuzorotesha uendeshaji wa Chama

    4. Kutoa taarifa na mapendekezo juu ya mapungufu mbalimbali yaliyojitokeza au yatakayojitokeza wakati wa uendeshaji wa Chama ili kiweze kuboresha utendaji wake na kuongeza tija na ufanisi.