IDARA YA WANAWAKE, AFYA NA USALAMA

    Utangulizi

    Idara inahusika katika kuratibu na kusimamia Wafanyakazi Wanawake, Wanachama na watu wenye Ulemavu. Idara inahamasisha Waajiri na Wafanyakazi kuzingatia na kudumisha Afya na Usalama kwenye maeneo ya kazi. Kupitia idara, Chama kimeweza kuunda Kamati zaidi ya 392 za Wanawake na zaidi ya Kamati 570 za Afya na Usalama Mahala pa Kazi.

    Kazi za Idara

    Idara inaratibu na kusimamia kazi zifuatazo;

    1. Kuendesha mikutano

    2. Kutoa Mafunzo na Elimu,

    3. Kupanga na kutembelea maeneo ya kazi,

    4. Kuhamasisha na kuingiza wanachama wapya,

    5. Kusimamia na kutekeleza Sera ya Wanawake, Afya na Usalama na Ukimwi,

    6. Kuhimiza waajiri kuweka mazingira safi na salama ya kazi na

    7. Kujenga na Kukuza katika kiwango cha juu masuala ya Afya ya Wafanyakazi Kimwili, Kiakili na Kijamii.

Baadhi ya Wafanyakazi Wanawake kutoka TUICO wakiadhimisha siku ya Wanawake Duniani