SEKTA YA HUDUMA & USHAURI

UTANGULIZI

Sekta hii ilianzishwa mwaka 2000 kwa ajili ya kutoa huduma kwa Wafanyakazi walio katika Kampuni na Taasisi zinazotoa huduma kwa jamii kama maji na usafi, shule binafsi, hospitali, Taasisi zisizo za Kiserikali (NGO’s), Taasisi za Kijamii (CSO’s) na wafanyakazi waliopo katika uchumi usio rasmi.

Kazi za Sekta

1. Kuwaunganisha Wafanyakazi na Mifuko ya Hifadhi za Jamii

2. Kushirikiana na Mashirikisho ya Vyama vya Wafanyakazi vya Kimataifa

3. Kutoa elimu ya ujasiriamali kwa Wanachama

4. Kuwaunganisha Wanachama na Taasisi zinazotoa Mikopo nafuu

5. Kuhamasisha Wafanyakazi walio katika uchumi usio rasmi kwa lengo la kurasimisha kutokana na mapendekezo ya Shirika la Kazi Duniani, Mkataba Na. 204

6. Kujenga na kudumisha ushirikiano wa utatu baina ya Chama, Serikali na Waajiri.

7. Kusimamia utekelezaji wa Mikataba, Maazimio na Matamko ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) yaliyoridhiwa na Nchi yetu.

8. Kushiriki katika Mabaraza ya Wafanyakazi

9. Kuhamasisha na kuingiza Wanachama wapya

10. Kushiriki katika mikutano mbalimbali ya wadau

11. Kuwakilisha wanachama katika utatuzi wa migogoro ya kikazi katika ngazi zote

12. Kujadili na kufunga mikataba ya hali bora (CBA) baina ya Chama na Waajiri