KITENGO CHA SHERIA

    Utangulizi

    Kitengo hiki kinasimamia masuala yote ya kisheria yanayokihusu Chama. Kina mawakili wa Mahakama Kuu wanaokiwakilisha Chama. Kitengo kinawakilisha wanachama katika Sekta zote za Chama kwenye Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) na Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi.

    Kazi za Kitengo

    1. Kuandaa nyaraka za Sheria

    2. Kukiwakilisha Chama katika mambo ya kisheria

    3. Kuwawakilisha Wanachama kwenye utatuzi wa migogoro ya kikazi

    4. Kushauri Chama kuzingatia na kutekeleza Sheria za Nchi katika utendaji wake

    5. Kushiriki kwenye Majadiliano ya pamoja na kufunga Mikataba ya Hali Bora

    6. Kutoa Elimu juu ya masuala ya Sheria kwa Wanachama na watumishi wa TUICO.

    7. Kuandaa mapendekezo juu ya marekebisho ya Miswada ya Sheria za kazi zilizopo.