Idara ya Elimu na uimarishaji

Utangulizi

Idara ya Elimu na Uimarishaji ilianzishwa rasmi mwaka 2001 kwa lengo la kuongeza na kuboresha Ujuzi, Maarifa, Zana, Vifaa na Nyenzo muhimu zinazohitajika katika shughuli za kutoa Elimu kwenye Chama. Idara hii inaratibu shughuli zote za Elimu za Chama. Katika kutekeleza majukumu yake, Idara inashirikiana na Wakuu wa Sekta, Wakuu wengine wa Idara na Vitengo kufuatana na Muundo wa Chama.

Kazi za Idara

Idara inatekeleza kazi zifuatazo;

1. Kutengeneza Makala za kufundishia

2. Kubuni na kuratibu Miradi ya Elimu ya Chama

3. Kuratibu shughuli zote za Elimu za Chama

4. Kuendesha Semina na Warsha kwa walengwa mbalimbali

5. Kuelimisha Waelimishaji (ToT) wa Chama

6. Kuratibu program zote za mafunzo zinazoendeshwa na Vyama vya Wafanyakazi vya Kimataifa

Watumishi wa TUICO wakiwa katika mafunzo ya TEHAMA.